Orodha Ya Majina ya Walioitwa Kwenye Mafunzo ZIMAMOTO May 2025

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linatangaza rasmi majina ya waombaji waliochaguliwa kuhudhuria mafunzo ya Uaskari ngazi ya Konstebo.

Tarehe ya Kuripoti Chuoni

Wote waliochaguliwa wanapaswa kuripoti katika Chuo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji – Chogo, Wilaya ya Handeni, Mkoa wa Tanga, kuanzia:

  • Tarehe: 16 Mei 2025 hadi 18 Mei 2025
  • Muda wa Mapokezi: Saa 12:00 asubuhi hadi saa 4:00 usiku

Mtu yeyote atakayeshindwa kufika ndani ya muda uliopangwa hatapokelewa, na nafasi yake itapewa mtu mwingine.

Maelekezo ya Usafiri

  • Shuka kituo cha Kabuku, ambacho kiko takribani kilomita 12 kutoka chuoni.
  • Chuo kimeandaa utaratibu wa kuwapokea waalikwa wote kuanzia tarehe zilizotajwa.

Gharama na Mahitaji ya Msingi

Mhusika anapaswa kujigharamia:

  • Nauli ya kwenda chuoni
  • Chakula na malazi hadi atakapopokelewa rasmi

Nyaraka Muhimu za Kuleta

Kila mhusika anapaswa kuja na:

  • Vyeti halisi vya masomo na taaluma
  • Cheti cha kuzaliwa
  • Kitambulisho cha NIDA au namba ya NIDA
  • Leseni hai ya udereva (kwa walioomba nafasi ya udereva)
    • Vyeti vyote viwe na nakala tatu (3) kwa kila kimoja.
    • Jina liwe sawa kwenye vyeti vyote—tofauti yoyote itasababisha kurejeshwa na nafasi kuchukuliwa na mwingine.

Ukaguzi wa Afya

Mhusika atapimwa:

  • Afya ya mwili
  • Afya ya akili
  • Kipimo cha mimba kwa wanawake
    Yeyote atakayebainika kuwa na matatizo ya kiafya hataruhusiwa kuendelea na mafunzo.

Vifaa vya Kuleta Chuoni

Mafunzo haya yanahitaji ulete vifaa vifuatavyo:

  • Mashuka 2 ya bluu
  • Mto 1 na foronya 2 za bluu
  • Chandarua cha duara rangi ya bluu
  • Ndoo ya plastiki (lita 20)
  • Sahani na kikombe cha bati
  • Fedha kidogo kwa matumizi binafsi
  • Bima ya afya (kwa waliyo nayo)

Vifaa vya kununua Chuoni

Vifaa vifuatavyo vitanunuliwa katika duka la chuo:

  • Raba za michezo
  • Fulana (T-shirt) ya rangi ya bluu
  • Madaftari makubwa (Counter books 4 quire – pcs 5)
  • Vifaa vya michezo (track suit, bukta ya bluu, fulana)
  • Kalamu

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linawapongeza waliochaguliwa na linatarajia ushirikiano mzuri katika hatua ya awali ya kujiunga na mafunzo.

Kupata Orodha ya Majina ya walioitwa Bonyeza HAPA!

Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti rasmi ya jeshi la zimamoto https://www.zimamoto.go.tz/

To apply for this job please visit www.zimamoto.go.tz.

Related Jobs